Jifunze Kiarabu - Utangulizi

Jifunze Uislamu
Jifunze Uislamu
8 هزار بار بازدید - 6 سال پیش - Hili ni darsa la kwanza
Hili ni darsa la kwanza la utangulizi katika mfululizo wa masomo ya Kiarabu yatakayotolewa na Shekh Nassor Ramadhan.

Darsa hizi zitafuata kitabu kinachoitwa DURUUSUL LUGHATUL  ARABIYYA kilichoandikwa na Dr. V. Abdulrahim. Kuna kitabu cha kiarabu kwa kiarabu na Kitabu cha kiarabu kwa kiingereza ambacho kinaitwa ARABIC COURSE for English Speaking Students cha Madina Islamic University.

Vitabu hivi vya kiarabu na kiingereza viko vitatu (Book 1,2 na 3) na ukivihitaji wasiliana nasi kwa +255625528326 au unaweza kutembelea maduka ya vitabu vya dini utavipata.

Walengwa wa somo hili ni wale ambao tayari wana uwezo wa kusoma kiarabu. Kama hujui kabisa kusoma maandishi ya kiarabu anza kusoma darsa za Jifunze Qurani zinazopatikana katika channel yetu hii hii.

Kwa maswali na maoni usisite kutuandikia kwenye comment box hapa chini.

Wassalam alaykum warahmatullah.
6 سال پیش در تاریخ 1397/03/29 منتشر شده است.
8,043 بـار بازدید شده
... بیشتر