KILIMO CHA MPUNGA IRINGA II

Kilimo Biashara
Kilimo Biashara
8.1 هزار بار بازدید - 5 سال پیش - Mradi wa RICE unaofadhiliwa na
Mradi wa RICE unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya ni moja ya jitihada za kupunguza changamoto ya upotevu wa mazao baada ya kilimo. Mradi huu unatekelezwa na Shirika la Chakula na Kilimo duniani (FAO) likishirikiana na serikali, halmashauri ya wilaya ya Iringa na Taasisi ya Maendeleo vijijini na Mijini (RUDI).

Lengo Kuu la mradi ni Kupunguza umaskini vijijini kupitia kuboresha ushindani wa wakulima wadogo wa mpunga katika sehemu ya ukanda wa SAGCOT.

Mradi huu unatekelezwa katika skimu kumi na Mbili (12) za Luganga, Magozi, Mkombozi, Mlenge, Makifu, Mafuruto,Idodi,Tungamalenga,Mlambalasi, Ipwasi Ndorobo na Makuka katika wilaya ya Iringa. Mradi unajenga uwezo wa viongozi wa vikundi vya wakulima ili kuweza kumudu vyema ushirikiano na wadau wengine katika mnyororo wa thamani na hivyo kuongeza uwezo wa kuhimili ushindani, kupunguza upotevu na kukidhi mahitaji ya soko.
5 سال پیش در تاریخ 1398/04/27 منتشر شده است.
8,159 بـار بازدید شده
... بیشتر