Tundu Lissu Aliamsha Dude Sakata la Mikataba ya Madini, Bunge Lachafuka

Global TV  Online
Global TV Online
913.2 هزار بار بازدید - 7 سال پیش - Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa tiketi ya Chadema ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa chama hicho, amekinukisha bungeni baada ya kusimama na kupinga kwa nguvu zote ripoti za kamati mbili za madini zilizoundwa na mheshimiwa rais huku akienda mbali zaidi na kusema kuwa zimejaa uchafu.
Lissu amefunguka kwamba uamuzi wa bunge kumpongeza mheshimiwa rais, si wa wabunge wote bali ni wa wabunge wa CCM kumpongeza mwenyekiti wao.
Akaendelea kwamba wajibu wa bunge ni kuishauri serikali na si kuisifia na kuiimbia mapambio, na kwamba ripoti ya kamati hizo mbili hazipaswi kusifiwa kwa sababu kabla yake, rais mstaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete waliunda kamati ambazo zilikuwa na mapendekezo bora zaidi.
Maneno makali ya Tundu Lissu, yaliamsha hasira kwa wabunge wa CCM ambao mara kwa mara walikuwa wakimzoea, hali iliyomfanya mwenyekiti wa bunge, Mhe Zungu awe na kazi ya ziada ya kutuliza hali ya hewa bungeni ambayo ilishachafuka.
Lissu amesema kwamba mpaka sasa, sheria zote zilizolifikisha taifa hapa lilipo, kuhusu madini, hakuna hata moja iliyorekebishwa ambapo kiwango kikubwa cha madini kinasafirishwa moja kwa moja kutoka kwenye migodi, jambo alilolifananisha na kuzuia mapanki wakati minofu inasafirishwa.
Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya…
uwazi1
uwazi1
uwazi1
WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/
FACEBOOK: Facebook: Globalpublishers
TWITTER: Twitter: GlobalHabari
INSTAGRAM: Instagram: globalpublishers
7 سال پیش در تاریخ 1396/03/24 منتشر شده است.
913,207 بـار بازدید شده
... بیشتر