Nyimbo za Sayansi! | Ubongo Kids - elimu burudani wa watoto

Ubongo Kids Kiswahili
Ubongo Kids Kiswahili
3.6 میلیون بار بازدید - 7 سال پیش - Imba nyimbo za sayansi na
Imba nyimbo za sayansi na wakina Mama Ndege, Anko T, Kibena, Kiduchu, Koba, Baraka na Amani! Jifunze kuhusu nishati ya sauti, mwanga, mwili, ukuaji, uzito na ujazo kupitia nyimbo za Ubongo Kids!

--

Jamani! Mwaka huu, Ubongo Kids ni ZAIDI ya hisabati na sayansi! Msimu huu si KAMA ULIVYOZOEA!

Ubongo Kids MPYA inamjenga mwanao, ikimpa fikra komavu zitakazomwezesha kutambua kusudi lake masomoni na maishani!

Njoo nasi Kokotoa, ukajifunze kutumia uwezo na utashi wako kusuluhisha changamoto zinazokukabili ili ufike pale utakapo!

Msimu wa 3 wa Ubongo Kids utakuandaa kifikra, ukichochea uwezo wako wa kung’amua matatizo na kuyatafutia ufumbuzi.

Ubongo Kids ni mfululizo wa hadithi za kusisimua zilizo katika mfumo wa elimu-burudani kwa ajili ya watoto wa miaka 7 hadi 13, zikitumia nyimbo na maudhui ya Kiafrika kuwafundisha hisabati na sayansi!

Katuni hii mahususi ya elimu inaandaliwa na Ubongo Learning, ambao pia ni watengenezaji wa kipindi murua ya AkiliandMe inayowaandaa watoto wa miaka 3-6 kwa ajili ya kwenda shule!

Tazama Ubongo Kids kila Jumamosi na Jumapili saa 3 asubuhi kupitia TBC1! Pata pia  webisodes zetu zote kupitia: http://www.ubongokids.com
7 سال پیش در تاریخ 1396/04/02 منتشر شده است.
3,650,408 بـار بازدید شده
... بیشتر