EACB NA SEMS APPAREL WAINGIA MAKUBALIANO KUTOA MAFUNZO YA UBUNIFU WA MAVAZI

WANAWAKE TV
WANAWAKE TV
80 بار بازدید - پارسال - #samiasuluhuhassan
#samiasuluhuhassan #biashara #ujasiriamali

Chuo cha East Africa College of Business (EACB) na Kiwanda cha Sems Apparel wameingia makubaliano ya ushirikiano katika kutoa elimu ya ushonaji wa nguo kwa rika mbalimbali hususan Vijana ili kuweza kujiajiri kupitia fani hiyo ya ushonaji.

Elimu hiyo itatolewa katika ngazi ya Certificate (Astashahada), Diploma (Stashahada) Degree (Shahada) kutoka kwa Wakufunzi waliobobea katika fani hiyo ya ushonaji wa nguo na ubunifu wa mavazi.

Vyuo vinavyotoa mafunzo kama hayo, Chuo cha Ufundi (VETA) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wametoa maoni yao kuhusu mafunzo hayo ambayo yatatolewa na EACB na Sems

Aidha, Wadau mbalimbali wanaohusika na ubunifu wa mavazi wametoa maoni yao kuhusu sekta hiyo ya ubunifu wa mavavi na ushonaji wa nguo kuingia kwenye mitaala rasmi ya kielimu.
پارسال در تاریخ 1402/05/10 منتشر شده است.
80 بـار بازدید شده
... بیشتر