Njia Kuu 5 Za Kuzuia Kompyuta Kutumia Sana Data

Learn Python
Learn Python
6.6 هزار بار بازدید - 5 سال پیش - DHIBITI MATUMIZI MABAYA YA MB
DHIBITI MATUMIZI MABAYA YA MB KATIKA KOMPYUTA.
Katika hii video tutajifunza njia kuu 5 za kudhibiti matumizi mabaya ya mb katika kompyuta, ikiwa ni sehemu ya kujibu maswali mengi kutoka kwa watumiaji tofauti wa kompyuta.
    Maswali yanayojibiwa na video hii.
1.  Kwanini Mb zinaisha haraka niki connect laptop yangu na internet.
2.  Njia zipi za kuzuia bundle/mb/data kuisha haraka katika kompyuta.
3. Ni kitu kipi hupelekea matumizi ya kupindukia ya mb katika kompyuta.
4. Kwanini mb katika kompyuta zinaisha bila mimi kutumia.
5. Njinsi ya kuzuia matumizi mabaya ya mb/data katika kompyuta.  

Katika hii video tutajifunza njia kuu 5 ambazo zitaondoa kabisa matumizi ya mb ya kupindukia katika kompyuta yako, kwanini uteseke, twende wote sambamba.

1. Automatically Windows Update.
Njia ya kwanza ya KUDHIBITI MATUMIZI MABAYA YA MB KATIKA KOMPYUTA ni hizi update za windows zilizosetiwa kufanya update kila mara kompyuta yako inapounganishwa na mtandao, hizi settings mara nyingi huwasumbua watu, hasa kwakufanya hizo update hata kama kompyuta imeunganishwa na hotspot au modem yenye mb kidogo.

2. Automatically Map Update.
Update za ramani ya dunia pia zimesetiwa kufanya updates mara kwa mara, na hii yote ni katika kuboresha mabadiriko yanayotokea katika ramani ya dunia, mfano ni kama nchi mbili zikijigawa na kuwa nchi mbili, lazima mabadiriko yawekwe katika ramani ya dunia, hivyo ili KUDHIBITI MATUMIZI MABAYA YA MB KATIKA KOMPYUTA, hizi settings unatakiwa kuziondoa.


3. Metered Connections.
Njia hii pia HUDHIBITI MATUMIZI MABAYA YA MB KATIKA KOMPYUTA, maana yake ni kwamba ukiseti wifi hotspot kama metered connection, ni kuuambia mfumo wako wa kompyuta kwamba una mb chache au kidogo, hivyo itumie taratibu.

4. Automatic File Upload.
Kama hii setting ipo on, itapelekea kompyuta yako kudownload files kama picha,documents, na video na kuzitunza kama akiba(backup) katika application kama OneDrive, hiki kitu si kizuri kwanini hupoteza sana mb katika kompyuta, unachotakiwa nikuzima hizi settings hili KUDHIBITI MATUMIZI MABAYA YA MB KATIKA KOMPYUTA.

5. Background Apps.
Hizi ni application ambazo hujianzisha, nyuma ya mfumo wa kompyuta, application hizo ni kama vile skype na twitter, hizi application humaliza mb kwa muda wote zinapokuwa active, hivyo ili  KUDHIBITI MATUMIZI MABAYA YA MB KATIKA KOMPYUTA, hizi settings unatakiwa kuziondoa.

Soma zaidi
https://www.motechapp.com/zuia-matumuzi/
Usisahau kusubscribe katika channeli yangu.

Kwa ushauri wowote wa IT(Information Technology)
           Follow me on Instagram : motech tz
           Follow me on Twitter : NoelDeMoses1
5 سال پیش در تاریخ 1398/06/13 منتشر شده است.
6,648 بـار بازدید شده
... بیشتر