JINSI YA KUPIGA WINDOWS 11 -INSTALL WINDOWS 11

Hakuna Matata Tech
Hakuna Matata Tech
670 بار بازدید - پارسال - Jinsi ya kupiga windows 11
Jinsi ya kupiga windows 11 au kufanya installation ya windows 11 (Install Windows 11 )Habari zenu , Leo nitakufundisha jinsi ya kupiga windows 11 kwenye kompyuta yako bila shida yoyote .

Katika funzo la leo utapata kujua hatua kwa hatua jinsi gani unaweza kuweka windows 11 yako kwenye kompyuta yako bila shida yoyote.

Sasa ili uweze kuweka windows kwanza lazima uwe na ISO file (Hii ni hatua ya kwanza) ISO file unaweza kupata kupita tovuti ya Microsoft wenywe wanakupa bure kabisa ila lazima ulipie namba za usajili wa windows.

Hivyo basi unaweza kudownload file lako la ISO ya windows 11 kutoka kwenye website yao Microsoft wenywe utaweza kupata hizo files za ISO.

Kama umepata file lako la ISO ya windows 11 inabidi uweke kwenye flash disk kwa njia inaitwa bootable flash hii itafanya flash disk yako au removable disk yako kua na uwezo wa kufanya boot kwenye kompyuta yako bila shida unaweza kutumia Application kama Rufus kwajili ya kuwezesha flash yako iwe bootable au unaweza kutumia pia Novi flash bootable hizi ni application ambazo ni free huitaji kulipia chochote.

Sasa baada ya kuweza kufanya vyote hivyo angalia video yetu hapo juu uweze kufanya installation ya windows kwenye kompyuta yako.
پارسال در تاریخ 1402/01/09 منتشر شده است.
670 بـار بازدید شده
... بیشتر