Fid Q - Tajiri Yangu Feat Paul Clement (Official Video)

Fid Q
Fid Q
216.1 هزار بار بازدید - 3 ساعت پیش - #FidQ
#FidQ #TajiriYangu #PaulClement #SlideDigital All praises due to the most high.. TAJIRI YANGU LYRICS: Verse 1: ( Fid Q ) Lord.. ni ngumu kujua wewe uko wapi ila unajua nilipo/ ninaisaka haki kuipata ni bahati na kwa waganga siko/ Vyuma vikikaza tunatangatanga kuuchanga mshiko.. na mbanga zinakwaza madada wakidanga wanabamba vifo/ Na waliopinda wewe huwalinda na love/ Ka wale wajinga ambao hunipinga ninapouwinda wokovu/ Haunipi shida bila namna ya kuisolve/ wewe ndio mmiliki wa kila tiba na hauna iliyo mbovu / Hauna iliyombovu.. unanipa uinchaji na power.. unaninyanyua juu/ Ni zaidi ya dawa.. sikuhitaji ninapougua tu/ Unaniweka sawa.. devil akitua hamchukui Q/ Una uwezo wa kunigawa au kuniumbua.. sio tu kuniumba mkuu/ ni rhumba tu ndio linaweka vumba juu na nakututesa kama mfungwa anayechungwa nakudundwa juu/ Wewe ndio BOSS ninayekuamini.. haututosi tukichomewa/ sio wale wanaowahi kazini ili wafoke tukichelewa... Chorus ( Paul Clement ) Ewe Ewe.. tajiri yangu/ Wewe ndiwe kila kitu kwangu/ Ewe Ewe tajiri yangu/ Wewe ndiwe kila kitu kwangu Ewe tajiri.. wa matajiri.. Ewe tajiri..Tajiri yangu/ Verse 2: ( Fid Q ) Mwanadamu amemtawala mwanadamu kwa kumuumiza/ Anakwapua mpaka asivyovihitaji bila kubakiza/ Hii inafanya nafsi yangu ikose subira/ Ikose usingizi, uoga., huzuni na hasira/ kwangu furaha ni kuwa na Mungu sio mlungura/ Na pia siku zote mla raha na uchungu hula/ Ninajua nilipotoka na ninajua wapi nilipo/ ispokuwa ni wewe pekee unajua lini nitafika mwisho/ cheo chako ni kirefu zaidi ya dunia... kipana zaidi ya bahari.. ulinzi mkali hakuna Askari anayefikia/ Ninamlaani shetani kiundani nipate kukujua mkuu/ ili nijihami na mtihani nisiache tusua Q/ Ninajua una huruma naomba nikibuma usinitose/ mwanadamu atazingua.. heshima sio utumwa kwa boss/ hawezi nunua uhai.. anajidai kwa lipi?/ na kwako sio tu akeshaye hata alalaye humpa riziki.. Chorus ( Paul Clement ) Ewe Ewe.. tajiri yangu/ Wewe ndiwe kila kitu kwangu/ Ewe Ewe tajiri yangu/ Wewe ndiwe kila kitu kwangu Ewe tajiri.. wa matajiri.. Ewe tajiri..Tajiri yangu Bridge ( Paul Clement ) Siwezi kuwa masikini sababu../ Anayenitunza ni tajiri.. ni Mungu/ Asiyeacha nigange njaa, nikosee furaha.. nikate tamaa/ eeh wee eeh wee tajiri yangu Chorus ( Paul Clement ) Ewe Ewe.. tajiri yangu/ Wewe ndiwe kila kitu kwangu/ Ewe Ewe tajiri yangu/ Wewe ndiwe kila kitu kwangu Ewe tajiri.. wa matajiri.. Ewe tajiri..Tajiri yangu FID Q Songs OUT WORLDWIDE ON MAJOR DIGITAL STORES: Written & Performed by Fid Q Follow Fid Q on: www.instagram.com/therealfidq/ twitter.com/FidQ Channel Administered by Slide Digital Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz
3 ساعت پیش در تاریخ 1403/07/17 منتشر شده است.
216,112 بـار بازدید شده
... بیشتر