Aliyepoteza wazazi wawili mauaji ya kimbari nchini Rwanda arejea kupiga kura

Mwananchi Digital
Mwananchi Digital
1 هزار بار بازدید - ماه قبل - Hesron Imanishimwe, ni Raia wa
Hesron Imanishimwe, ni Raia wa Rwanda Leo Jumapili Julai 14, 2024, amesimulia madhira ya maisha aliyokumbana nayo baada ya kupoteza wazazi wake wote wawili sambamba na ndugu zake wengi mwaka 1994 wakati wa mauaji ya kimbari.

Anasema hakuwa na fikra kama kuna siku atarejea tena Rwanda kutokana na upweke alionao baada ya kupoteza ndugu zake.

Imanishimwe anasema wakati mauaji hayo yanafanyika, alikuwa na miaka saba na alilazimika kuishi kwenye nyumba zilizokuwa zikihifadhi watu wasio na makazi zilizotolewa na Serikali ya Rwanda kwa kuwa hakuwa na mahali pa kuishi.

Hata hivyo, anasema baada ya kumaliza shule, akili ilimjia ya kusaka makazi mahala pengine nje ya Rwanda.

Anasema aliamua kufanya hivyo ili kuepuka kuyaona mazingira yaliyopoteza ndugu zake wote.

Hivyo, anasema katika kusaka ni mahali gani angeweza kuishi kwa amani, akaamua kukimbilia Nairobi ambako alianza maisha upya.

Anasema mara nyingi aliwazia hali ingekuwa vipi endapo angerejea tena Rwanda.

Hata hivyo anasema hali haiku kama alivyokuwa anawaza na sasa ameamua kuja kupiga kura kwenye uchaguzi huo mkuu unaofanyika kesho Jumatatu, Julai 15, 2024.

Video Credit ‪@Kiswahili‬
ماه قبل در تاریخ 1403/04/24 منتشر شده است.
1,020 بـار بازدید شده
... بیشتر