Mkuu wa mkoa wa Mwanza aagiza watumishi wanne kusimamishwa kazi

Mwananchi Digital
Mwananchi Digital
2.5 هزار بار بازدید - 2 سال پیش - Mwanza. Mkuu wa mkoa wa
Mwanza. Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Adam Malima ameagiza kuwasimamisha kazi watumishi wanne waliohusika katika tuhuma za kuuza ardhi namba. 194 na namba 195 vyenye thamani ya Sh1 bilioni vilivyopo Rwegasore kata ya Sahara wilaya ya Nyamagana huku maamuzi ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Sekiete Yahya ikiachiwa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI kumchukulia hatua za kinidhamu.

Watumishi waliosimamishwa ni Mhahasibu wa Jiji, Mwanasheria, Afisa Manunuzi, na Afisa Mipango ili kupisha uchunguzi zaidi endapo wamehusika katika mauzo ya viwanja hivyo viwili vinavyodaiwa kuwa na thamani kubwa kuliko iliyouzwa, huku hatua za kinidhamu kwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza zikisubiliwa kutolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI baada ya kupata barua kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Akizungumza na vyombo vya habari hapo jana jioni, Malima amesema watumishi hao wanne wameshirikiana na Mkurugenzi wa Jiji  kuuza ardhi hiyo huku Mkurugenzi akibainika pia kufanya maamuzi bila kufuata utaratibu, kukiuka maadili ya viongozi kwa kukiuka maelekezo ya kamati ya ulinzi na Usalama, mkuu wa wilaya na maelezo kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa.
2 سال پیش در تاریخ 1401/10/23 منتشر شده است.
2,504 بـار بازدید شده
... بیشتر